Pages

Pages

Tuesday, June 18, 2013

Mabomu yaanza kurushwa tena jijini Arusha na kusababisha mkanyaganao wa watu, taharuki



Na Mwandishi Wetu, Arusha
HALI ya usalama jijini Arusha imezidi kutoweka baada ya mabomu yameanza kupigwa muda huu, jambo linalowafanya watu wakimbie ovyo, kufuatia na jeshi la Polisi kuzuia mikusanyiko ya watu, hasa katika kipindi hiki cha maombolezo ya vifo vya watu wawili katika mkutano wa kampeni wa Chadema, chini ya mwenyekiti wao Freeman Mbowe.
Hayo ni maendeleo ya vuta nikuvute ya serikali na wananchi hasa waliokuwa upande wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, ikiwa ni siku chache kabla ya bomu kurushwa katika Mkutano wa Kampeni ya Chadema, huku ukihutubiwa na mwenyekiti wao, Mbowe.
Matokeo hayo pia yalisababisha Uchaguzi Mdogo wa udiwani katika kata nne jijini Arusha kusogezwa mbele hadi Juni 30 mwaka huu, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha kwamba usalama unakuwa wa kutosha katika jiji hilo la kibiashara.

Jana, serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, alitangaza kauli ya serikali, ikienda sambamba na kutenga Milioni 100 kwa ajili ya mtu atayetaja mtandao wa ulipuaji mabomu katika Taifa hili.

Mbowe aliwaambiwa wandishi wa habari kuwa bomu lililorushwa katika mkutano wao lilirushwa na Polisi, jambo ambalo hata hivyo linapingwa vikali, zaidi ya kusubiria taarifa ya kiutalaamu wa Polisi.

Watu wawili walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa, mlipuko ambao umeanza kuchukuliwa kirahisi kutokana na baadhi yao kuanza kuingiza siasa za maji taka.

No comments:

Post a Comment