Pages

Pages

Tuesday, June 18, 2013

Watu watatu wahofiwa kufa leo jijini Arusha, wakati wabunge watatu wa Chadema wakamatwa na Mbowe atimua mbio



Na Mwandishi Wetu, Arusha
WATU watatu wamedaiwa kufa leo jijini Arusha, baada ya kutokea machafuko yaliyosababisha upigwaji wa mabomu na wananchi kuzagaa ovyo mitaani. Aidha zipo taarifa kuwa Mbunge Tundu Lissu amevunjika mguu katika pilika pilika hizo.
Hali ilivyokuwa jijini Arusha leo.
Mwandishi wetu jijini Arusha alitupasha kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kilikuwa kikifanya mkutano bila kupewa kibali maalum kutoka polisi, ikiwa ni siku moja baada ya kuzuiwa kukusanyika bila utaratibu.

Wabunge wanne wa Chadema, wamekamatwa na polisi kutokana na kufanya mkutano wao katika Uwanja wa Soweto bila kupata kibali kutoka jeshi la Polisi.

Kamishina wa Polisi Paulo Chagonja, alisema viongozi wa Chadema waliokamatwa ni pamoja na Tundu Lissu, Mustafa Akoonay, Said Arf na Joyce Nkya, huku Freeman Mbowe akifanikiwa kutimua mbio.

Kwa siku kadhaa sasa jiji la Arusha limekuwa kwenye mshike mshike wa aina yake, huku hatua za awali zikisema kuwa bomu lililorushwa katika Mkutano wa Chadema limetengenezwa nchini China.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alitembelea majeruhi  na wafiwa katika jiji la Arusha, huku akisema kuwa serikali itagharamia kwa kiasi kikubwa juu ya mahitaji ya walioathirika na bomu hilo pamoja na kugharamia pia mazishi ya waliofariki.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limemtaka Mbowe awasilishe haraka ushahidi juu ya mtu anayehusika na ulipuaji wa bomu kama alivyotangaza mwenyewe baada ya mlipuko huo.

No comments:

Post a Comment