Pages

Pages

Friday, June 21, 2013

Chadema yaitunishia msuri serikali, Jeshi la Polisi kwa kugoma kupeleka ushahidi na kutaka Tume Huru ya kimahakama



Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe mwenye miwani akiwasili Polisi jana.

Freeman Mbowe wa pili kutoka kulia, akijadiliana jambo baada ya kujisalimisha Polisi.

Na Mwandishi Wetu, Arusha
HALI ya mvutano kati ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), pamoja na Jeshi la Polisi, unaendelea kushika kasi huku mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akiwa mkali kama mbogo na kusema kuwa hawezi kuwasilisha ushahidi wa mlipuko wa bomu kwa polisi isipokuwa kwa Tume Maalum ya kimahakama.

Madai ya Mbowe yamepokelewa kwa hisia tofauti, huku wale wasiounga mkono harakati za wapinzani wakichukulia kama njia ya kulisumbua jeshi la Polisi pamoja na kutafuta umaarufu mbele ya jamii.

Jana Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alitangaza hali ya hatari kwa wananchi watakaokaidi agizo halali la jeshi la Polisi, jambo litakalosababisha polisi watumie nguvu, ikiwapo kuwatandika virungu.

"Wapigwe tu, maana ndio njia halali ya kutuliza vurugu, hivyo nashauri wananchi wasiwe wakaidi maagizo halali ya Polisi," alisema Pinda na kuzua maswali kwa wananchi hasa waliokuwa upande wa Chadema.



Mwenyekiti wa CHADEMA Fremaan Mbowe pamoja na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kushoto kwake walipojisalimisha Polisi jana.

No comments:

Post a Comment