Pages

Pages

Friday, June 21, 2013

Benki ya CRDB kununua wimbo wa THT uitwao FahariHuduma



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENKI ya CRDB imetangaza kuununua wimbo uitwao ‘Fahari Huduma’ ulioimbwa na msanii Mataluma pamoja na taasisi ya kukuza na kulea vipaji ya Tanzania House of Talents THT.
          Mataluma  wa THT akiwajibika jukwaani.
CRDB walitangaza uamuzi huo kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji, Charles Kimei, katika uzinduzi wa huduma mpya ya benki kwa kupitia mawakala itakayosambazwa nchi nzima kama sehemu ya kuwasogezea Watanzania huduma za kuweka na kutoa pesa.
THT wakifanya manjonjo yao.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, kwenye uzinduzi huo, Kimei alisema amefurahishwa kwa jinsi wimbo huo ulivyoimbwa na unavyochezwa, hivyo ameagiza watu wake wa masoko waununuwe haraka iwezekanavyo ili usiweze kutumiwa na wengine.

Alisema kuwa endapo wimbo huo hautanunuliwa, unaweza kutumiwa na makampuni mengine, wakati ni maalum kwa ajili ya benki yao ya CRDB.

“Kwakweli nimefurahishwa kwa kiasi kikubwa na wimbo huu, hivyo watu wangu wa masoko lazima make chini na taasisi hii ili muununuwe ili usitumiwe tofauti na sisi CRDB.

“Unaweza kuitambulisha vyema huduma yetu hii ya benki kwa njia ya wakala, ambapo mteja anaweza kutoa na kuweka pesa, bila kusahau wale wanaolipa bili mbalimbali kwa kupitia mawakala wetu,” alisema Kimei.

Huduma hiyo ya Fahari Huduma inatarajiwa kupokewa vizuri na Watanzania, ukizingatia kuwa itakuwa wamesogezewa karibu huduma za kibenki kwa njia ya mawakala badala ya matawi ya benki, kama ilivyozoeleka wakati huu.

No comments:

Post a Comment