Pages

Pages

Saturday, June 01, 2013

Bajaj mpya yenye ubora zaidi yazinduliwa jijini Dar es Salaam leo


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Shinyanga Emporium (1978), leo imezindua Bajaj mpya aina ya Piaggio ambayo haitumii mafuta mengi, hivyo kuwa mkombozi kwa wananchi wote, wakiwamo wafanyabiashara wa Bajaj.
 Nishit Peter, Meneja wa Tawi lililopo karibu na Mlimani City, akitoa maelekezo kwa wateja wake waliotembelea kwenye  uzinduzi wa bajaj aina ya Piaggio, leo jijini Dar es Salaam.

Tunasikiliza kwa makini.
 Hii ni nzuri sana.
Nishit Peter, Meneja wa Tawi lililopo karibu na Mlimani City, akitoa maelekezo kwa mteja wake katika uzinduzi wa bajaj aina ya Piaggio, leo jijini Dar es Salaam.

Tukio la uzinduzi wa bajaj hiyo lilifanyika leo mchana katika tawi lao lililopo karibu na Mlimani City, likihudhuliwa na watu mbalimbali, wakiwamo wafanyabiashara wa bajaj jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Biashara wa Kampuni hiyo, Ritesh Monani, alisema kuwa bajaj hiyo ni mkombozi kwa watu wote, hasa matumizi yake mazuri ya mafuta, ikitumia lita moja kwa kilomita 32, huku tenki lake likiwa na uwezo wa kubeba lita 10.

Alisema bajaj hiyo kwa sasa inapatikana kwa Shilingi Milioni 5.7, ambapo mteja atafurahia mpangilio mzima wa uundwaji wake, sambamba na upatikanaji wa vipuri vyake Tanzania.

“Tumekuwa tukipokea maoni ya wateja wetu Tanzania, hivyo bajaj hii ni nzuri kwa watu wote, jambo linalotupa imani kuwa itapokelewa kwa mikono mizuri sambamba na usalama wake,”alisema.

Usafiri wa bajaj hutumiwa sana duniani, hasa nchini India, huku kwa jijini Dar es Salaam, ukijulikana kama moja ya usafiri unaomuwezesha mtu kufika haraka anapokwenda.

No comments:

Post a Comment