Pages

Pages

Sunday, June 02, 2013

Green Stone wajiandaa na uzinduzi wa tawi lao baadaye mwaka huu


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TAWI la Yanga la Green Stone lenye maskani yake Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, linajipanga kufanya uzinduzi rasmi wa tawi lao baadaye mwaka huu.
Yusuphed Mhandeni, waliosimama wa tatu kutoka kushoto mstari wa nyumba.

Tawi hilo limepatiwa usajili rasmi kutoka Makao Makuu ya klabu yao ya Yanga, huku likishirikisha watu mbalimbali, akiwamo mwimbaji wa muziki wa taarabu nchini, Khadija Kopa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, mlezi wa tawi hilo, Yusuph Shaban Mhandeni, maarufu kama (Yusuphed Mhandeni), alisema kuwa wanajipanga kulizindua rasmi tawi lao kwa kushirikisha wadau wengi wa Yanga pamoja na viongozi wa juu.

Alisema wanaamini kwa kufanikisha hilo, watajiweka katika mzani mzuri katika sekta ya michezo, kwa kujichanganya na wanachama wenzao kwa ajili ya kuisaidia timu yao ya Yanga.

“Tunajiandaa na uzinduzi rasmi wa tawi letu baadaye mwaka huu kwa ajili ya kukutanisha wanachama wote wanaotokea Green Stone na kujuana na wadau wenzao wa mpira wa miguu.

“Naamini mpango huu utakuwa na tija ukifanikiwa, maana kubwa ni kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda vizuri, ukizingatia kuwa tayari tumeshajiweka katika mazingira mazuri katika sekta ya michezo hapa nchini,” alisema Yusuphed Mhandeni.

Tawi la Green Stone linaongozwa na mwenyekiti wake, ambaye pia ni msanii nyota wa filamu hapa nchini, Lumolwe Matovolwa, maarufu kama (Big).

No comments:

Post a Comment