Pages

Pages

Sunday, May 19, 2013

Wazee wa Ngwasuma hapatoshi leo New Msasani Club



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi ya FM Academia, Wazee wa Ngwasuma, imesema kuwa inafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa mashabiki wao wanapata burudani kamili kutoka kwao, kwa kufanya mambo makubwa jukwaani.
                     Rais wa FM Academia, Nyosh El Sadaat

Ngwasuma wamerejea hivi karibuni kutoka kwenye ziara zao za mikoani, ambapo Jumapili ya leo wanafanya shoo yao katika Ukumbi wa  New Msasani Club, jijini Dar es Salaam.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Kelvin Mkinga, alisema kuwa vijana wao wamejipanga imara kuhakikisha kuwa mashabiki wao wanapata vitu adimu kutoka kwao.

Alisema katika ziara zao za mikoani walizomaliza wiki iliyopita, wadau wao walifanikiwa kuona uwezo wao na jinsi vijana wanavyolishambulia jukwaa bila kuchoka.

“FM Academia ni bendi ya kazi, hivyo kila mtu anayetaka kupambana na sisi anapaswa kujipanga imara, ukizingatia hatuna muda wa kupoteza wa kubishana kwa namna moja ama nyingine.

“Kila kitu kinawezekana, ndio maana kila mwanamuziki wetu amejipanga imara kufanya shoo ya aina yake katika kumbi mbalimbali tunazokuwapo na kufuta ubishi wa kuwa na mpinzani hapa nchini,” alisema.

FM Academia inayofanya shoo ya kila Jumapili katika Ukumbi wa New Msasani Club, inaongozwa na Rais wa Vijana, Nyosh El Sadaat, akishirikiana na wakali wengine, akiwamo Patcho Mwamba.

No comments:

Post a Comment