Pages

Pages

Sunday, May 19, 2013

Khadija Kopa naye aongozwa Miss Ukonga



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa taarabu nchini, Khadija Kopa, ameongezwa katika utoaji burudani katika fainali za Miss Ukonga 2013, zinazotarajiwa kufanyika Mei 25, katika Ukumbi wa Wenge Club, jijini Dar es Salaam.
                                          Khadija Kopa
Warembo hao kwa sasa wanafanya mazoezi makali katika Ukumbi wa Hill Tech, Ukonga, huku wakijifua vilivyo kuhakikisha nao wanatoa burudani za aina yake katika usiku huo wa Redds Miss Ukonga.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa shindano hilo, Chiku Chambuso, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea, ikiwa ni kumalizana na mwimbaji huyo wa taarabu, atakayeshirikiana kwa pamoja na Banana Zoro na bendi yake ya B-Bendi.

Alisema kuwa anaamini kuwa burudani za mwimbaji huyo wa taarabu na wengineo watafanya mambo makubwa katika shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wao.

“Kutakuwa na burudani za aina yake katika shindano hili ambalo mabinti wenye uwezo wa kucheza na jukwaa wanajifua vilivyo katika kuhakikisha kuwa mambo yao yanakuwa mazuri.

“Naamini kila kitu kitakuwa sawa katika kuhakikisha kuwa mabinti wanafanya mambo makubwa kwenye shindano letu la Miss Ukonga 2013 lenye ushindani wa kila aina,” alisema.

Wadhamini wa shindano hilo ni Redds, Z-Entertainment, UEFA go Pub, Break Point, Salut 5, Mamushka Bar, Hilltech resolt, Kiota Jungle, Business Times, Times FM na Clouds FM.

No comments:

Post a Comment