Pages

Pages

Sunday, May 19, 2013

Vurugu kubwa zaibuka Iringa Mjini, mabomu ya machozi yaendelea kurushwa na polisi



Na Mwandishi Wetu, Iringa
HALAI si shwari Iringa mjini baada ya kutokea vurugu kubwa kati ya Jeshi la Polisi na wafanyabiashara mjini hapa na kusababisha taharuki ya aina yake.
            Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa           
Machafuko mpaka sasa ni makubwa mno maeneo ya Mashine Tatu barabara zimefungwa, maduka yamefungwa na hakuna kinachoendelea zaidi ya machafuko hayo.

Watu wanaendelea kuchoma matairi barabarani na kupopoa kwa mawe kwenye  magari ya polisi wanaohangaika kutuliza ghasia kwa kutumia mabomu ya machozi.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, juzi alisikika akikemea vurugu za serikali kwa kupitia jeshi lao na kuwaambia kuwa wasinyanyase raia kwenye jimbo lake.

Bado juhudi za Polisi zinaendelea katika kuhakikisha kuwa vurugu hizo zinakoma na kurudi kwenye utulivu wake wa kawaida.

No comments:

Post a Comment