Pages

Pages

Friday, May 24, 2013

Wananchi 200 mjini Mtwara wadaiwa kukimbia nyumba zao, jengo moja lalipuliwa leo Msimbati



Na Mwandishi Wetu, Mtwara
KUTOKANA na machafuko yanayoendelea mjini Mtwara, wananchi zaidi ya 200 wamedaiwa kukimbilia kijijini Naliendele ili kupumzika kwa maswahibu yanayoendelea katika mji huo, chanzo kikiwa ni kugombania gesi isisafirishwe.
                         Picha na maktaba yetu.
Kwa siku tatu sasa mji wa Mtwara umefurika askari polisi na jeshi kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi kutokana na mgogoro huo na kulazimisha kupigwa kwa mabomu na watu kadhaa kupoteza maisha yao.

Mwandishi wa Handeni Kwetu, aliyopo mjini Mtwara alisema kuwa wananchi wengi wameamua kuuhama mji huo kwasababu ya kuhofia usalama wao.

“Kumekuwa na ongezeko kubwa la uchomaji wa nyumba za wananchi pamoja na wizi unaoendelea kuwaacha wananchi kwenye wakati mgumu mno, hivyo wengi wao wameamua kukimbilia sehemu nyingine,” alisema.

Kutokana na askari wengi kumwaga mjini Mtwara, pilika pilika zimetulia, ingawa ni sehemu chache zilizosikika milipuko, ukiwapo mtaa wa Msimbati, ambako jingo la Marine Park lililipuliwa.

No comments:

Post a Comment