Pages

Pages

Thursday, May 23, 2013

Diamond: Nalinga kwasababu najua mapenzi na nawamudu wanawake



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII nyota wa kizazi kipya, Nassib Abdulmalick, maarufu kama Diamond, amesema kuwa analingia kitendo cha kuyajua vyema mapenzi jambo linalomfanya kila binti achenguke kuwa naye.
 Diamond, a.k.a Sukari ya warembo
Diamond akizungumza na mwanadada Sporah
Diamond kwa sasa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanadada Penny, penzi ambalo lilizua gumzo kubwa hapa Tanzania, kufuatia tabia yake ya kutoka kimapenzi na mabinti wengine kwa kipindi kifupi.

Diamond aliyatoa hayo katika kipindi cha Sporah akiwa nchini Uingereza, ambapo alishindwa kujizuia na kuanza kusifia kuwa yeye ni mkali wa kuwapet pet, yani kuwalainisha mabinti kwenye majambozi.

Najua sana kupet pet, hilo namshukuru Mungu, hivyo ndio maana huwa nazua gumzo katika suala zima la uhusiano wa kimapenzi na wasichana,” alisema Diamond, anayetamba katika game Bongo.

Wimbo wa Diamond unaotikisa kwa sasa ni ule wa Nataka Kulewa, pamoja na ule aliyoshirikishwa na Ney wa Mitego unaokwenda kwa jina la Muziki Gani, wimbo ambao umezidi kuwaweka juu kimuziki.

No comments:

Post a Comment