Pages

Pages

Saturday, May 11, 2013

Wambura achekelea kuitwa Kamati ya Mipango Simba


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ALIYEKUWA mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Michael Wambura, amepokea kwa furaha kuitwa kwenye Kamati ya Mpango Mkakati ya klabu ya Simba, huku akisema kuwa hana ugomvi wala mgogoro na klabu ya Simba.
Michael Richard Wambura
Mbali na Wambura, uteuzi huo pia umewahusisha watu mbalimbali, akiwamo Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, ambao wote kwa pamoja wameingizwa kwa ajili ya kufanya juhudi za kuipatia maendeleo klabu hiyo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Wambura alisema kuwa amepokea kwa furaha uteuzi huo kwasababu hana mgogoro na wanachama wala viongozi wa klabu ya Simba, hivyo yupo tayari kutoa ushirikiano wake wakati wowote unapohitajika.

Alisema kuwa klabu ya Simba inahitaji mipango na uendelezaji, hivyo kitendo cha kuundwa kwa Kamati hiyo ni sehemu ya kuikomboa Simba ambayo kwa sasa inakabiriwa na changamoto za aina yake.

“Nashukuru kwa viongozi wa Simba kuona kuwa nafaa kuwapo kwenye kamati hiyo mpya ambayo naamini kwa pamoja tutafanya kazi kwa ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya klabu kwa ujumla.

“Sina mgogoro na mtu yoyote kwenye suala la michezo hususan mpira wa miguu, hivyo kwa sasa akili yangu yote ni kujaribu kutoa mawazo mazuri kwa ajili ya maendeleo ya soka Tanzania,” alisema Wambura.

Joseph Itang’are, Swedy Mkwabi, Francis Waya, Ramesh Patel, Evance Aveva, Mulamu Ng’hambi, Salim Mhene, Mtemi Ramadhani, Moses Basena, Henry Tandau, Omary Gumbo, Michael Wambura, Glory Nghayomah, Crensencius Magori, Honest Njau, Ruge Mutahaba, Evodius Mtawala na  Dr Mwafyenga.

No comments:

Post a Comment