Pages

Pages

Saturday, May 11, 2013

Matukio ya awali sherehe za kuzaliwa mtoto Rahimu Kambi Mbwana leo jijini Dar es Salaam

Hii ni keki maalum kwa ajili ya Rahimu Kambi Mbwana. Hakika ni kudhihirisha kuwa leo ametimiza mwaka mmoja tangu kuzaliwa kwake. Natumia fursa hii kumtakia kheri na baraka katika maisha yake pamoja na wote waliozaliwa siku ya leo.



 Rahimy Kambi Mbwana mwenye t-shirt yenye mistari akiwa tayari kwa keki na mazaga zaga mengine yaliyoandaliwa maalum kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa. Umeona eheee. Ilikuwa ni shangwe zaidi ya sana katika maeneo yake ya kujidai. Happy Birthday Rahimu Kambi Mbwana.



 Rahimu Kambi Mbwana akiwa amebebwa na shangazi yake Rehema Mbwana kulia na Zaina Mbwana kushoto kwake kwa ajili ya kumuandaa kisaikolojia juu ya sherehe fupi. Hiyo ilikuwa ni dakika chache baada ya kutoka usingizini. Ilikuwa balaa tupu. Watu walimsubiri hadi alipoamka. Kwanza alikuwa hataki kuvaa hiyo kitu kichwani kwake. Sijui alijua ni nini?



 Hata kama nisipokuwapo leo duniani, lakini naamini Rahimu Kambi Mbwana atakuwa kwenye mikono salama kama anavyoonekana hapo kushikwa na shangazi zake wakimpa hili na lile. Kulia ni Rehema Mbwana na kushoto ni Zaina Mbwana. Wote hawa ni shangazi zake na walikuwapo home kujumuika pamoja.

 Burudani za aina yake kama unavyoona.


Hapo vipi? Ndivyo wanavyouliza hawa baada ya kuwekwa kwa ajili ya kusubiri utaratibu wa keki na vinywaji vingine vilivyoandaliwa katika siku ya kuzaliwa ya Rahimu Kambi Mbwana aliyetimiza mwaka mmoja tangu kuzaliwa kwake. Picha zote na Mpigapicha wa Handeni Kwetu blog.

No comments:

Post a Comment