Pages

Pages

Saturday, May 11, 2013

Kila asiyejua mapenzi akiachwa, basi wataachwa wengi



MAMBO FULANI MUHIMU

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI jambo la busara mno kama wewe ni mpenzi wa safu hii kiasi cha kuwa na mimi kila Jumamosi kama ya leo. Hakika, wewe unanifanya niendelee kuwapo hapa kuelimishana, kupeana hili na lile katika suala zima la uhusiano wa kimaisha na mapenzi.
                                                     Uhusiano
Ndugu msomaji wangu mpendwa, watu tunatofautiana sana katika kila kitu kwenye mambo ya kimaisha. Katika suala hilo, wapo ambao wana mapungufu ya kila aina.

Kwa mfano, katika uhusiano na maisha, kuna watu ambao suala la utundu katika mapenzi si asili yao. Ni wazito kiasi cha kuwafanya wapenzi wao, wake au waume zao kukerwa nao.

Kwa bahati mbaya, upungufu huo unageuka kuwa haki ya wenzao kuwasaliti kisa wanahitaji wasichana au wavulana wepesi, watundu na wanaojua mambo ya mapenzi.

Si sahihi na jambo hilo linatakiwa lipingwe kwa namna moja ama nyingine, maana kama kila asiyejua mapenzi ana haki ya kuachwa, basi wataachwa wengi mno.

Wasiokuwa na uwezo au utundu wa kuwatosheleza wenzao kwasababu hawajui mchezo huo ni wengi kulingana na mahitaji ya jamii au wale waliokuwa kwenye uhusiano nao.

Kutokana na hilo, unapokuwa kwenye uhusiano na mtu ambaye umegundua kuwa hana uelewa kwenye suala zima la mapenzi, hakika unapaswa kulichukulia jambo muhimu mno.

Usimuache eti kwasababu hakutoshelezi au hufurahii lolote unapokuwa naye. Kinyume cha hapo, jamii inapaswa ikulaumu, maana hadi kugundua kuwa uliyekuwa naye hakutoshelezi, si mjuzi wa mapenzi, ina maana wewe ni hodari zaidi yake.

Kwa sababu hiyo, jinsi ulivyokuwa wewe, unaweza kumfundisha mbinu nyepesi na rahisi kwa hatua ya kwanza na baadaye mpenzi au mke wako atakuwa mwenye kukupa kile kinachostahili.

Dawa si kumuacha, maana hata hao utakaokutana nao m bele ya safari wanaweza kuwa wazito zaidi ya uliyokuwa naye awali. Utaacha wangapi? Je, kama wewe ndio hujui ukiachwa utafurahi?

Nimekuwa nikipata maswali ya kila aina kutoka kwa wasoamji wangu, huku mbinu gani, au malalamiko ya watu wasiojua mapenzi kwenye uhusiano likichukua nafasi kubwa.

Kwa sababu hiyo, kila mtu anapaswa kumfungia kazi aliyekuwa naye katika hali yaa kuhakikisha lazima awe mjuzi. Nasema hivi maana si vibaya kumuelekeza mtu wako.

Na wale wanaoelekezwa nao lazima wajuwe kuwa jambo hilo linatokana na wapenzi wao, wake au waume zao kuhitaji kuwa nao kwa kipindi kirefu, hivyo wakubali kwa roho moja.

Kuna wale ambao wakifufundishwa au kuelekezwa kulingana na mahitaji ya watu wao, huwa wanyonge au kulalamikika kuwa wamedharauliwa na watu wao.

Wengine hufika mbali kwa kuanza kuwachukia watu wao, au kuwaona ni wahuni maana suala hilo wamejifundishia wapi? “Niondolee uhuni wako, haya mambo wewe umeyajulia wapi,”? ni kauli inayotoka katika baadhi ya vinywa vya watu wakiwaeleza wapenzi wao, jambo linalozalisha kukata tamaa kwa wenzao.

Badala ya kusema hayo, watu ambao hujitolea kuwaelekeza wapenzi wao, huwa na lengo la kuwaweka katika nafasi nzuri, ili wajuwe namna ya kukabiriana na suala zima la uhusiano wa kimapenzi.

Ingawa kweli wapo watu ambao hawatosheki kiasi cha kutoka nje kila siku, lakini ni tofauti na wale wanaotoka au kuwa na wengine kwasababu hawatoshelezwi na watu wao.

Wale wasiotoshelezwa ni rahisi sana kutoka nje wakiangalia kuwa waliokuwa nao majumbani mwao au kwenye uhusiano hawana mbinu za kuwatoa kijasho.

Ni jambo la kujiuliza kwa kina. Je, mimi na wewe tunapokuwa kwenye mambo ya wakubwa wapenzi wetu, wachumba wetu, wake au waume wanapokeaje uwepo wetu?

Je, wanafika kileleni au ndio tumekuwa wazito, tukikimbia hatua moja tumechoka, hatutaki kuendelea hivyo kuwaacha wenzetu katika hali mbaya kiasi cha kufikia kutamani wengine?

Wehenga wamesema, usipojenga ufa, basi utajenga ukuta.
Tukutane tena wiki ijayo.
0712 053949
0753 806087

No comments:

Post a Comment