Pages

Pages

Monday, May 20, 2013

Malkia wa urembo, Miss Moshi apatikana, ni Winlady White





 


 Mlimbende Winlady White Mushi ndie aliyefanikiwa kunyakua taji la Redds miss Moshi 2013. 

Hawa ndio warembo waliofanikiwa kuingia  tatu bora kwenye Redds Miss Moshi 2013 ambapo washindi hawa ndio wataiwakilisha wilaya ya moshi katika kumsaka Miss Kilimanjaro 2013.


WINLADY WHITE MUSHI (20), Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika biashara, Chuo cha Biashara na Ushirika Moshi (MUCCoBS), mshiriki namba 1, ametawazwa kuwa malkia mpya wa urembo Moshi mjini, Redds Miss Moshi 2013.
White mwenye ndoto za kuwa mbunifu wa kimataifa, huku ikiwa ndio mara yake ya kwanza kushiriki ulimbwende, alifanikiwa kutwaa taji hilo na kumrithi Redds Miss Moshi 2012, Angela Filbert.

Timu ya majaji watano wakiongozwa na Jaji mkuu, Jaji Brian walimtawaza Malkia huyo akiwabwaga wapinzani wake, Veronica Chami, Martha Charles, Winnie Macha na Ester Freddy.


sema kwa kuzingatia vigezo vyote vya mashindano ya ulimbwende vinavyotumika kitaifa na kimataifa wote kwa pamoja waliridhika na kila walichokishuhudia kabla ya kuamua kumtangaza Wnlady White kuwa Redds Miss Moshi mwaka 2013.

 
Washindi wengine ni, Mshindi wa pili, Mshiriki namba 9, Veronica Chami, (1st runner up), mshindi wa Tatu, mshiriki namba 3, Esther Freddy (2nd runner up), mshindi wa 4, mshiriki namba 15, Martha Charles (3rd runner up) huku nafasi ya tano ikienda kwa mshiriki namba 13, Winnie Macha (4th runner up).

Adija Ibrahimu, ambaye ni mshiriki namba 6, alitangazwa kuwa Miss Talent 2013, akimbwaga mpinzani wake wa pekee mshiriki namba 4, Jacky Mushi ambaye tangu mwanzo wa kinyanganyiro alikuwa anapigiwa upatu wa kuchomoka na taji hilo.


Hawa ndio walimbende walioingia  tano bora kwenye Redds miss Moshi 2013 na kupata nafasi za kuweza kuulizwa na kujibu maswali ili kuweza kuwapata washindi watatu ambao wataiwakilisha wilaya ya moshi.
 


Winlady White Mushi ambaye ndio Redds miss Moshi 2013/2014 akijibu swali.
 

Hawa ni baadhi ya warembo wa Redds kutoka katika wilaya tofauti tofauti mkoani Kilimanjaro ambao wataungana na warembo wa Redds Miss Moshi 2013 katika mtanange wa kumsaka Miss Kilimanjaro 2013.
 

Winlady White Mushi "Redds miss Moshi 2013/2014" akionyesha kipaji chake na hapo alikua akicheza nyimbo yenye mahadhi ya kihindi.
 
Huyu ndio aliyekuwa Redds Miss Moshi 20122/2013 akisubiri kumkabidhi taji Redds Miss Moshi 2013/2014.
 
Presenters wa Redds Miss Moshi 2013/2014 wakiwa na washiriki wa Redds Miss Moshi waliofanikiwa kuingia tatu bora.

Hawa walikua ni baadhi ya wanafunzi kutoka chuo cha MUCCoBS wakishangilia kwa furaha baada ya Winlady White Mushi kutangazwa kuwa ndio mshindi wa Redds miss Moshi 2013/2014 ambaye mshiriki huyo ni mwanafunzi katika chuo cha MUCCoBS.
Dully Sykes aliyepamba jukwaani kazi ni moja tu....kutoa burudani....

 Presenter Kasim Mwinyi aka Babi D'e Conscious akifanya yake.


Redds Miss Moshi 2013, iliyofanyika katika ukumbi wa Aventure mjini Moshi, yalidhaminiwa na Redds Original, Panone and Company Ltd, Bonite Bottlers, Baba G, A n A Boutique na Zoom net Printers
                                                         

No comments:

Post a Comment