Pages

Pages

Sunday, May 05, 2013

Titanic yaendelea kutamba Nachingwea


Na Said Hamdani, Lindi
TIMU ya Titanic FC ya mjini Nachingwea, imeiadhibu Vijana SC kutoka wilaya ya Liwale, baada ya kuichapa mabao 4-2 mchezo wa ligi ya Taifa ngazi ya mkoa hatua ya makundi,uliofanyika uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea.

Kwa mujibu wa msimamizi wa kituo hicho,Said nandonde,Titanic ndio walikuwa wa kwanza kupata mabao ya kuongoza yaliyowekwa wavuni na Hassani Amour katika dakikaya 11 na 19.

Nandonde alisema kutokana na kufungwa kwa mabao hayo, Vijana SC waliamka usingizini na katika dakika ya 25 Vijana SC walijipatia bao kwanza lililofungwa na Hassani Mchite.

Aidha,alisema kufungwa kwa bao hilo kuliwafanya Titanic kuongeza kasi na katika dakika ya 27 mchezaji Abdurahamani Rashidi aliifungia bao la tatu, ambayo yalidumu hadi wakati wa mapumziko.

Vijana FC waliendelea kujitutumua na katika dakika ya 38 mchezaji Aikosi Mpwate aliiandikia timu yake bao la ipili na la mwisho kwa upande wao.

Titanic FC waliendelea kuliandama lango la wapinzani wao na katika dakika za 62 na 88 mchezaji Awadhi Mohamedi alifunga kalamu ya mabao kwa kuweka kimiani mabao mawili.

Hadi mwisho wa mpambano huo,Titanic ilitoka uwanjani ikiwa na ushindi wa mabao 4-2.

Kwa matokeo ya kituo hicho, Titanic inaongoza kwa kuwa na pointi tatu na magoli sita ya kufunga na kufungwa manne,ikifuatiwa na New Generation iliyo na pointi tatu na magoli matat ya kufunga na kufungwa mawili.

No comments:

Post a Comment