Pages

Pages

Sunday, May 05, 2013

Cheka: Sipo tayari kufanyiwa upasuaji wa mkono wangu


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Francis Cheka, amesema kwamba hayupo tayari kufanyiwa upasuaji wa mkono wake kwa siku za hivi karibuni, kutokana na kuogopa kujipa matatizo makubwa katika sekta ya masumbwi Tanzania.
 

                       Francis Cheka, bondia wa Tanzania
Juzi Cheka aliibuka na ushindi baada ya kumtandika bila huruma Thomas Mashali na kuendeleza ubabe wake kwa mabondia wa Tanzania kutokana na kuwapa kipondo kila wakati.

 Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Cheka alisema haoni sababu ya kuacha masumbwi kwasababu ya kufanyiwa upasuaji wa mkono wake ulioanza kumletea matatizo.

Alisema katika kipindi chake cha masumbwi, anaamini akiamua kufanyiwa upasuaji wa mkono huo, hali yake kimaisha itakuwa mbaya, hasa kama mkono utamsumbua na kushindwa kupanda ulingoni.

“Upasuaji ni kitu kigumu na hakika kama nitafanyiwa upasuaji naweza kuwa nje ya ulingo kwa kipindi kirefu, ndio maana sipo tayari juu ya hilo.

“Nitaendelea kufanya mazoezi na maajabu kwa kuwapiga kila anayepita mbele yangu, maana ngumi ni moja ya vitu ninavyomudu kwa kiasi kikubwa na hakika nimedhamiria juu ya hilo,” alisema.

Cheka ni miongoni mwa mabondia wanaofanya vyema katika sekta ya masumbwi na kuitangaza vyema Tanzania nje ya mipaka yake kutokana na kushinda kwa kila pambano analopanda ulingoni.

No comments:

Post a Comment