Pages

Pages

Sunday, May 05, 2013

Bomu laripuka uzinduzi wa Kanisa jijini Arusha na kuzua taharuki


HABARI kutoka jijini Arusha zinasema kuwa kuna bomu limeripuka katika Kanisa la Parokia Mpya ya Olasiti na kuzua taharuki ya aina yake.
Habari zinasema kuwa Kanisa hilo lilikuwa linazinduliwa leo wakati waumini kanisa hilo walikuwa wakiendelea na sherehe zao za uzinduzi huo, huku lishangaza watu wengi, ingawa haijajulikana madhara ya mripuko huo.

Taarifa za awali zinasema kuwa kuna gari lilifika hapo na kushuka mtu ambaye baadaye bomu hilo lilisikika likiripuka na kuleta mkanganyiko kwa waumini waliokwenda kufanya uzinduzi huo wa Kanisa.

Taarifa zaidi zitaendelea kukujia kadri zitakavyoendelea kupatikana kutoka mjini Arusha.


No comments:

Post a Comment