Pages

Pages

Sunday, May 26, 2013

Niyonzima: Siwezi kucheza soka Simba


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KIUNGO wa timu ya Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kwamba amekosa kabisa hamu ya kukipiga katika klabu ya Simba, ndio maana aliweza kuwakatalia akijua kuwa bado ana lengo la kuendelea kuwa mwajiriwa wa Jangwani.
 Haruna Niyonzima katikati akiwa na viongozi wa Yanga
 Juzi uongozi wa Yanga ulitangaza kumuongezea mkataba wa miaka mwili mchezaji huyo ambaye anapendwa na mashabiki wengi katika klabu hiyo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Niyonzima alisema kuwa kila mchezaji ana ndoto zake, hivyo yeye kucheza Simba ni moja ya vitu ambavyo hawezi kuviweka mbele hata kidogo.

Alisema ingawa timu nyingi zilikuwa zikimuwinda, ila ndoto za kucheza Simba hakuwa nazo na hawezi kubadili uamuzi wake, ingawa mpira ni pesa na lolote linaweza kutokea.

“Nilijua kuwa mkataba wangu upo mwisho, ila kubwa nilitamani kuendelea kuwapo Yanga kwa msimu mmoja zaidi, ndio maana hata wale niliokuwa nazungumza nao sikuwapa ushirikiano.

“Mchezaji anayewika uwanjani kufuatiliwa ni jambo la kawaida, ila ni vyema katika suala hilo mtu kufanya uamuzi wa busara na wenye maslahi katika maisha yake ya mpira wa miguu,” alisema.

Baada ya kuongeza mkataba wake kwa miaka misimu miwili zaidi, Niyonzima anajiandaa kurudi kwao nchini Rwanda, kabla ya kurejea baadaye kuendelea na kibarua chake mitaa ya jangwani.

No comments:

Post a Comment