Pages

Pages

Sunday, May 26, 2013

Extra Bongo: Tunajipanga upya kiburudani



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya Extra Bongo, maarufu kama Next Level, Wazee wa Kiziguo, imesema kuwa baada ya kusukiwa zengwe katika viwanja vya Garden Breeze, Magomeni, sasa wanajipanga kutafuta sehemu nyingine ili kuendeleza bonanza lao kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wao.
Ally Choki, Mkurugenzi wa Extra Bongo
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mapema wiki hii, Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki, alisema kuwa sehemu hiyo ikipatikana wataendelea na bonanza lao la kila Jumapili.

Alisema kuwa awali bonanza lao la Magomeni lilikuwa na wapenzi wengi, ndio maana mahasimu wao kimuziki waliona ugumu wa kupambana nao na kujikuta wakianza kuwatafutia namna ya kuwaathiri.

“Kwa sasa tunachofanya ni kutafuta namna ya kurudisha bonanza letu katika sehemu nyingine, ingawa tunafahamu kuwa tulipotoka tulisukiwa zengwe kwa ajili ya kuiathiri bendi yetu.

“Hatuwezi kuangalia hilo, zaidi ya kujipanga zaidi kwa ajili ya kuendeleza harakati zetu kimuziki, ukizingatia kuwa tulianzisha bonanza kwa ajili ya kukutanisha wadau wote sehemu moja,” alisema Choki.

Extra Bongo mbali na kuwa na Choki kama Mkurugenzi, pia imekusanya wanamuziki wenye uwezo wa kutisha, akiwamo Rogati Hega Katapila, Ramadhan Masanja Banza Stone, Athanas, Khadija Kimobiteli na wengineo.

No comments:

Post a Comment