Pages

Pages

Wednesday, May 29, 2013

Msiba wa Ofisa Habari wa Bunge, Ernest Zulu wazua utata, ndugu waanza kuvutana kabla ya maziko yake


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HALI ha hatari imejitokeza katika msiba wa Ofisa Habari wa Bunge, Ernest Zulu, baada ya jana usiku kutokea mvutano kutokana na upande mmoja kalazimisha aende kuzikwa kwao Songea, huku watoto wakitaka azikwe jijini Dar es Salaam.
Marehemu Ernest Zulu kulia enzi za uhai wake.
Kabla ya kifo chake, marehemu alitoa usia kuwa akifa basi azikwe jijini Dar es Salaam alipozikwa motto wake wa kwanza, hata hivyo kaka wa marehemu, Emmanuel Zulu, amekuja juu akitaka mdogo wake akazikwe nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa mama wa marehemu, Telesia Zulu, yeye ametakiwa na daktari asisafiri safari ya mbali kutokana na kupata ajali kubwa hivi karibuni.

Aidha mtoto wa kwanza wa marehemu, Phelemona alisema msiba huo umekuwa na utata kwasababu ya ndugu wanaofosi baba yake akazikwe Songea.

Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila alilazimika kufanya kikao cha masaa zaidi ya matatu na ndugu wa marehemu kujaribu kutafuta namna ya kuweka sawa mambo hayo.

Zulu anatarajiwa kuwasili leo kutoka nje ya nchi alipokuwa anasoma, ambapo msiba wake umedaiwa kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya kichwa na kupelekea kufanyiwa upasuaji.

No comments:

Post a Comment