Pages

Pages

Wednesday, May 29, 2013

Kifo cha Mangwea chatikisa nchi, mipango ya kuleta mwili wake yawekwa


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAJONZI. Kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya akiwa nchini Afrika Kusini, Albert Mangwea, kimeendelea kutikisa vichwa vya watu wengi hapa nchini, huku Shirikisho la Muziki Tanzania likitoa tamko kwa mara ya kwanza.


Mangwea enzi za uhai wake
Wasanii mbalimbali, akiwamo Mrisho Mpoto, Afande Sele na wadau wengine kila mmoja anaelezea kwa mtazamo wake kifo cha Ngwea kilichotikisa hisia zao.


Akizungumza mapema leo asubuhi, Rais wa Shirikisho la Muziki nchini, Addo Novemba, alisema kuwa kifo cha msanii huyo ni pigo zito katika tasnia ya muziki nchini.

Alisema kuwa uwezo wake na aina ya kifo chake kimesababisha maswali na majonzi makubwa katika tasnia hiyo inayoeendelea kuchanua siku hadi siku hapa nchini.

“Tunawapa pole wazazi, ndugu, jamaa na watanzania kwa kuondokewa na Mwanamuziki huyo Nguli wa kizazi Kipya huku tukimkumbuka kwa mengi, hasa msimamo aliouonesha katika mambo anayoyaamini.

“Marehemu alitambulika sana katika tasnia ya kizazi kipya kwa kupitia wimbo wa GHETO LANGU TU ba baadae nyimbo zake nyingi na staili yake ya kughani ilipendwa,” alisema na kuongeza.

“Tunawaomba watanzania wazidi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu, Shirikisho lenu lipo Imara na tutashiriki kikamilifu katika msiba huu, tutawapa taarifa zaidi ya siba kadiri muda unavyokwenda, Mungu ibariki Afrika,” alisema.

Shirikisho hilo linasema linaendelea kufanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa msanii huyo analetwa Tanzania kwa ajili yaa kuandaa taratibu za maziko yake, mara baada ya familia kujua namna gani ya kuustiri mwili wa mpendwa wao.

Aidha, rafiki ya Mangwea anayejulikana kama M 2 The P  naye ameripotiwa kufariki Dunia na kuungana na swahiba wake.

No comments:

Post a Comment