Pages

Pages

Wednesday, May 29, 2013

Mapya yaibuka Afrika Kusini baada ya kugundulika kuwa M 2 the P hajafa, juhudi za kuuleta mwili wa Ngwea zaendelea kushika kasi



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HABARI mpya juu ya tukio la msiba wa Albert Mangwea zinaendelea nchini Afrika Kusini, huku habari zikikanusha kifo cha msanii mwingine aliyekuwa na Ngwea, anayejulikana kwa jina la M 2 the P.


Ngwea kushoto na M 2 the P walipokuwa nchini Afrika Kusini.
Taarifa hizo zinaonyesha kuwa msanii huyo hajafa, huku juhudi zinazofanywa kwa sasa ni kufanikisha kuuleta mwili wa Mangwea. Msiba wa Ngwea kwa sasa upo nyumbani kwa kaka yake Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Ngwea atazikwa nyumbani kwa mama yake mkoani Morogoro na harakati za wadau zinafanywa ili kupata fedha za kugharamia kuletwa kwa mwili wa msanii huyo aliyefanya vyema katika tasnia ya Bongo Fleva, kabla ya kifo chake.


Albert Mangwea aliariki Dunia nchini Afrika Kusini katika Hospitali ya Helen Joseph ya jijini Johanesburg alipopelekwa baada ya kugunduliwa na wenzake asubuhi kwamba alikuwa hoi.
Hali hiyo ilimkuta maeneo ya Brixton-Mayfair West ambapo alikuwa amefikia kwa rafiki yake ambaye walisoma wote miaka ya nyuma.

No comments:

Post a Comment