Pages

Pages

Sunday, May 12, 2013

Miss Tanzania 2012 ajitetea kutojua lugha ya Kiswahili na kuwatupia zigo la mavi wabunge wanaomcheka


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MISS Tanzania mwaka 2012, Brigitte Alfred, amewajia juu wabunge wanaomcheka kwa madai kuwa hajui Lugha ya Kiswahili kwa kuwaambia hawana hoja zaidi ya kusema ili wasikike katika majukwaa ya kisiasa kwa kuwatoa wenzao kafara.
Miss Tanzania (2012), Brigitte Alfred
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog Ijumaa iliyopita, Brigitte alisema sio kweli kuwa hawezi kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili kama wanavyosema baadhi ya wabunge.

Alisema kuwa anachokumbuka ni kutumia lugha ya kingereza baada ya kuandika speech yake, jambo ambalo lilitafsiliwa kuwa ni kutojua lugha yake ya Taifa.

“Sitaki kusikiliza maneno ya wabunge maana ni wanasiasa, ila najua lugha ya Kiswahili, lakini wakati mwingine mtu anaweza kukosea au kufanya kile ambacho hakifurahishi baadhi yao.
 
“Sikujua kuwa kuzungumza lugha ya kingereza ningesemwa na kutajwa ovyo ovyo, maana pamoja na kujua vyema lugha yangu, ila wakati mwingine nakuwa mwamuzi wa mwisho wa cha kuzungumza na lugha nitakayoitumia maana zote nazijua,” alisema Brigitte.

Maneno ya Mrembo huyo yaliyotokana na swali aliloulizwa kuwa ni lugha gani anaipenda kuizungumza na kujisikia yupo sawa au lugha ambayo hawezi kuizungumza mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment