Pages

Pages

Saturday, May 11, 2013

Handeni Kwetu Blog inakutakia kheri na baraka kutimiza mwaka mmoja tangu kuzaliwa kwako, Rahimu Kambi Mbwana


Baada ya shughuli kuendelea ya Birthday ya Rahimu Kambi Mbwana, hayupo pichani, mama mtu, Grace Misango ilifikia zamu yake kuwalisha keki watoto waliokuja kumpa kampani mshikaji wao. Duh. Ilikuwa bonge la burudani kutoka pande hizi.


 Tunasubiri magaza zaga jamani. Ndivyo wanavyosema hawa wadau waliokuja kwenye shughuli fupi ya Birthday ya Rahimu Kambi Mbwana, mwenye t-shirt yenye mistari mistari. Meza ilichafukaje?


 Duhhhhhhh. Umeona nini hapa? Mshumaa umelipuliwa kidizaini hivi.Watu wanashangilia. Kila mmoja na furaha tele. Ilikuwa burudani za aina yake. Kwakweli wote tulifurahia kuimba wimbo maalum kwa ajili ya Rahimu Kambi Mbwana, mbele ya meza, aliyeshikwa wakati mshumaa unawaka na kuleta shangwe za aina yake.


Kadri muda ulivyokuwa ukienda, ndivyo mtu alivyopandwa na mzuka. Mwenyewe akaanza kucheza muziki na kuwaacha watu hoi. Kama anavyoonekana hapo Rahimu mwenye t-shirt yenye mistari mistari akicheza na wenzake wakati akifurahia siku yake ya kuzaliwa.



Watu weweeeeee. Rahimu Kambi Mbwana amepandwa na mzuka sasa. Anaruka kwanja kwa jwebda mbele. Nikasema sijui ndio ameshaanza kuonyesha kipaji chake. Usiniambie kuwa jamaa anataka nafasi za watu kwenye sanaa ya muziki Tanzania.

 Tunacheza kwa raha zetu jamani
 Kama kawaida jamani


Natumia fursa hii kumpongeza Rahimu Kambi Mbwana kwa kutimiza mwaka mmoja tangu alipozaliwa siku kama ya leo jijini Dar es Salaam. Nakutakia kila la kheri katika kipindi cha maisha yako duniani mtoto wangu mpendwa.

No comments:

Post a Comment