Pages

Pages

Wednesday, May 15, 2013

Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015, Wema Sepetu adaiwa kujiwinda kuwania Ubunge



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HABARI zilizopenyezwa kutoka katika ngome ya malkia wa Tanzania, Wema Abraham Sepetu, zinasema kuwa nyota huyo anayetingisha Bongo yupo kwenye mipango ya kujitosa kwenye siasa kwa kuwaza nafasi ya Ubunge ili akashiriki kutunga sheria mjengoni.
                                  Wema Sepetu, pichani
Hata hivyo, haijabainika kuwa dada huyo anataka ubunge kwa njia gani, ikiwamo kugombea katika majimbo Tanzania, au viti maalum kutoka katika vyama mbalimbali vya siasa.

Mdau wa ndani kabisa na Wema alisema “Ni dhahiri dada anataka Ubunge na hakika nitamuunga mkono kama anavyoniambia kila wakati, japo najua atapata upinzani wa kutosha.

“Ubunge ni moja ya nafasi nyeti serikali maana atakuwa kwenye kundi la wanaotunga sheria bungeni pamoja na kuwa na nafasi kubwa ya kuwatumikia Watanzania wenzake,” alisema mpashaji huyo.

Hata hivyo, simu ya Wema haijapatikana moja kuweza kuitolea ufafanuzi taarifa hiyo iliyoingia katika meza ya Handeni Kwetu mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni kati ya taarifa ya kushtua kwa mwanadada huyo.

Kwa siku za hivi karibuni, vijana mbalimbali wakiwamo wasanii wamekuwa na hamu kubwa ya kujitosa katika siasa katika sehemu mbalimbali, huku wakiongozwa na Joseph Mbilinyi, Sugu, ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema.

No comments:

Post a Comment