Pages

Pages

Friday, May 10, 2013

Kaseba: Nitamdunda Rasco Simwanza

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA mwenye uzito wa kutisha, Japhet Kaseba, amesema amejipanga imara kuhakikisha kuwa anamdunda mpinzani wake Rasco Simwanza katika Ulingo wa DDC Magomeni Kondoa, June 8 mwaka huu.
Japhet Kaseba, Bondia wa Tanzania
Pambano hilo linafanyika huku Watanzania wakiwa na imani kubwa na bondia huyo aliyewahi kuwika pia kwenye ulingo wa ngumi za mateke, Kick Boxing na kuwa Bingwa wa Dunia.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema kuwa kwa sasa anajifua vilivyo kulinda nguvu zake dhidi ya mpinzani huyo anayetokea nchini Malawi.

Alisema lengo lake ni kuhakikisha kuwa anaitangaza vyema nchi kwa kumpiga Simwanza anayekuja Tanzania akiwa na nia moja ya kumtia aibu nchini kwao.

“Sitakubali kumuacha Simwanza afanye lolote baya katika mwili wangu,hivyo naomba wadau wa ngumi wasubiri kuona shangwe zinapatikana ukizingatia kuwa uwezo wangu ni mkubwa dhidi ya bondia huyo kutoka Malawi.

“Nitampiga katika hali yoyote ile, ukizingatia kwamba nafanya mazoezi makali kwa ajili hiyo, hivyo Simwanza ajiandaye kuja kwa furaha na kurudi kwao kwa huzuni,” alisema.

Kaseba amepania vilivyo kuona anashinda katika pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa masumbwi hapa nchini, wenye hamu ya kuona mabondia wao wanafanya vizuri ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment