Pages

Pages

Friday, May 10, 2013

Kuelekea mechi ya watani wa jadi Mei 18, wazee Yanga watoa tamkoa zito


Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wazee wa YANGA, Napenda Kuwafahamisha kuwa Wazee wa YANGA wamefurahi na kuwashukuru Viongozi wa Klabu ya YANGA chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji na Makamu Mwenyekiti Clement Sanga kwa kuongoza Klabu na kuweza kunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa mwaka 2012/2013. Ushindi huu umetokana na Uongozi bora, uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya Klabu na kufikia malengo.
Ibrahim Akilimali kushoto akizungumza  na baadhi ya wazee wa klabu ya Yanga. Picha na Maktaba ya Handeni Kwetu Blog.

Mwenyekiti wetu ametujengea dhana ya kuwa na imani ndani ya Uongozi, wanachama na wachezaji wetu.

Hivyo basi na sisi kama wazee wa Klabu tunayo imani na viongozi na wachezaji wetu na tunaahidi kuwa mchezo wetu wa tarehe 18 Mei 2013 kati yetu na Simba lazima tushinde ili tusherehekee Ubingwa wetu kwa furaha, shangwe na nderemo.

“YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”

K.n.y: YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB na MWENYEKITI WA WAZEE                                       YANGA ALHAJ JABIRI M. KATUNDU

Naomba kuwasilisha.

IBRAHIM O. AKILIMALI
KATIBU WA WAZEE WA YANGA

No comments:

Post a Comment