Pages

Pages

Friday, May 10, 2013

Wasanii kibao kushiriki Made in Tanzania mjini Dodoma kesho Jumamosi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASANII wengi wanatarajiwa kuhudhuria kwenye tukio la ‘Made in Tanzania’ lenye kauli mbio ya ‘Twenzetu Dodoma’, linalotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi mjini Dodoma na kuandaliwa na Kampuni ya Clouds Media Group.
Wema Sepetu, msanii wa Bongo Movie
Twenzetu Dodoma ni mpango maalumu wa kuwakutanisha watu mbalimbali wakiwamo wasanii ambao nao wataitumia siku hiyo kutafakari mafanikio yao kwa kuangalia fursa wanazokutana nazo.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alisema kuwa lengo la kushiriki kwenye program hiyo ni kutafuta fursa ya kimaisha, kwa watu mbalimbali wakiwapo wasanii Tanzania.

Alisema watu wengi wamekubali kushiriki kwenye siku hiyo ya Made in Tanzania, akiwapo Selemani Msindi Afande Sele, Wema Sepetu na wengineo.

“Hii ni siku nzuri kwa watu wote kuangalia namna gani tunaweza kutafuta fursa ya kimaisha, wakiwapo wasanii ambao kila siku wamekuwa watu wa kulalamika kuwa wanaibiwa haki zao.

“Watu wataanza kuelekea Dodoma Ijumaa ya leo ambapo tunaamini mpango huo utafanyika kesho Jumamosi katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma,” alisema.

Tukio hilo linafanyika kwa mara ya kwanza ikiwa ni mpango wa kuwaweka sawa vijana kwa ajili ya kuangalia namna gani ya kujiendeleza kimaisha kwa kutumia fursa wanazokutana nazo.


No comments:

Post a Comment