Pages

Pages

Sunday, May 05, 2013

Familia yalia baba yao, msanii wa Bongo Movie kutelekezwa baada ya kugongwa na gari

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ aligongwa na gari wakati akifanya mazoezi ya kutembea kufuatia ugonjwa wake wa kiharusi.

Tukio hilo lilitokea Aprili 21, mwaka huu maeneo ya Kariakoo, Dar ambapo gari hilo aina ya Toyota Voxy lilitokea ghafla na kumgonga kidogo na kumsababishia michubuko miguuni na kichwani.

Dereva wa gari hilo alifanya uungwana kwa kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi ambapo ndugu zake walitaarifiwa na kwenda kumchukua.

“Mzee Kankaa alitoka nyumbani na kuwaaga kuwa anakwenda kufanya matembezi. Walijua ni karibu, lakini baadaye tukasikia taarifa kuwa amepata ajali na yupo Kituo cha Polisi Msimbazi,” alisema Abdul ambaye ni mtoto wa Kankaa.

Kuangalia mzee kama huyu katangaza sana kazi ya sanaa ya Tanzana lakini saizi hali yake sio nzuri au tunasubilia siku yaza msiba kuonesha ufahari wa kutoa michango pamoja na kuuza sura. Wengi wamefanyiwa hivyo sasa tubadilike Watanzania wenzangu.

No comments:

Post a Comment