Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Clouds FM,
imejitolea kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwea kwa ajili ya kuutoa
Afrika Kusini hadi Tanzania kwa ajili ya kuzikwa, ukiwa ni utaratibu unaoonyesha kuwa wadau wote wameamua kushirikiana katika suala hili.
Barua inayoonyesha walioanza kuchangia msiba wa Ngwea
Mkurugenzi wa Utafiti na
Matukio wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, alithibitisha kuchukua uamuzi huo kwa
ajili ya kufanikisha mazishi ya nyota huyo wa Bongo Fleva.
Marehemu Albert Mangwea
Taarifa za Kampuni hiyo
kusaidia zilianza kuenea tangu juzi, baada ya Kamati ya Mazishi kushindwa
kutaja makampuni, taasisi na watu walioanza kuchangia kwenye msiba huo.
Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
"Tumeamua kwa mikono miwili
kushiriki katika msiba huu wa ndugu yetu Mangwea,” alisema kwa ufupi.
Ngwea amepangwa kuletwa
Tanzania kesho Jumamosi na kuagwa Jumapili, kabla ya kupelekwa mkoani Morogoro
kwa ajili ya mazishi yake.