Pages

Pages

Thursday, May 30, 2013

Watanzania wapewa namba za kuchangia msiba wa Ngwea na huku ikitangazwa kuwa ripoti zilizosambaa jana juu ya kifo chake ni za uongo



 Namba za Mchango wa Msiba ni 0754 074323 au 0658 074324.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMATI ya Mazishi ya msanii Albert Mangwea aliyefia nchini Afrika Kusini, imewataka Watanzania wote kuungana juu ya kufanikisha kuuleta mwili wa msanii huyo na kufanikiwa kuuweka kwenye nyumba ya milele.
Hayo yamesemwa leo mchana jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Kamati hiyo, Adam Juma, ambaye pia ameshirikiana na Shirikisho la Muziki Tanzania, chini ya uongozi wake Addo Novemba.

Juma alisema kuwa gharama ni kubwa mno kuuleta mwili huo, hivyo wadau na taasisi kwa pamoja washirikiane ili kuhakikisha kuwa msanii huyo analetwa na kuzikwa mkoani Morogoro.
 Tusiachiwe sisi peke yetu na wala hakuna sababau ya kuwatenga wengine kaatika suala hili maana Ngwea amefanya kazi kwa pamoja na watu wengi, hivyo hapa lazima tuungane,” alisema Juma.

Naye Novemba alisema kuwa kwa kawaida gharama za msiba huo ni kubwa, maana wamepanga waulete Jumamosi na kulala Hospitali ya Taifa Muhimbili, huku Jumapili wakitarajia kuuaga kwenye Uwanja wa Leaders Club, jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya hapo wataupeleka Morogoro kwa ajili ya maziko.

Kuna vitu vingi vilivyopangwa ambavyo vyote vinahitaji gharama, hivyo hatuwezi kukataa msaada wa mtu yoyote yule, maana ana haki kama binadamu au Mtanzania,” alisema Novemba.

Hata hivyo, jana kwa mahesabu ya haraka haraka, Novemba aliweka wazi kuwa zaidi ya Milioni 30 zinahitajika kwa ajili ya kufanikisha uletwaji wa marehemu na maziko yake.

Kamati ya Mazishi imemjulisha wasanii mbalimbali, akiwamo Noorah, TID, Profesa Jay, P-Funk, pamoja na kaka wa marehemu, Kenneth Mangwea.

Kwa yoyote anayetaka kuchangia alichokuwa nacho kwa ajili ya kufanikisha msiba huo anatakiwa achangie kwa namba 0754 074323 au 0658 074324.
Msiba wa Ngwea kwa sasa upo nyumbani kwa kaka yake, Mbezi Beach, maeneo ya Goigo. Aidha, Kamati imetangaza kuwa habari zozte za ripoti za kifo cha Ngwea zilizosambazwa jana sio za kweli, maana zimebuniwa na watu wanaotaka kumchafua marehemu.

No comments:

Post a Comment