Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UCHACHE wa wadau na mashabiki wa bendi ya The African Stars
Twanga Pepeta katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, umeanza kutia hofu
wadau wake, baada ya jana shoo yao kuhudhuriwa na watu wachache, huku Salehe
Kupaza akishindwa kuwapo kwenye onyesho lao.
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka
Kupaza hakuja kwenye shoo hiyo ya bonanza la kila Jumapili
kwa madai kuwa anaumwa, ingawa zipo tetesi kuwa mwanamuziki huyo tegemeo kwa
Twanga Pepeta ana mpango wa kutimka mapema mwaka huu kwa ajili ya akutafuta
maisha zaidi.
Vipaza sauti vyetu vilivyotegwa vilivyo katika viwanja hivyo
vilinasa mazungumzo ya huruma kutoka kwa wadau haswa wa Twanga Pepeta,
wakionyesha wasiwasi mkubwa kutokana na mwenendo mbovu na uchache wa mashabiki
wao.
“Sehemu kama hii ilikuwa haikamatiki kutokana na watu kuwa
wengi kiasi cha wengineo kutumia kujiimarisha kiuchumi kwa kuleta biashara zao
mbalimbali, lakini sasa kuna haja ya kuangalia kwingine kwenye mwitikio wa
watu.
“Si kila anayekuja kwenye bonanza kama hili anakuja
kustarehe, wengine wapo kibiashara, sasa kama hali hii itaendelea, kuna haja
wenye bendi wajipange kabla ya mambo hayajakuwa mabaya zaidi,” alisema mdau
huyo kwa masikitiko makubwa.
Mbali na uchache huo, lakini Handeni Kwetu haikushindwa
kuwanasa wadau mahiri wa Twanga Pepeta, wakiwamo viwanjani hapo kupata
burudani, akiwamo Mathew Kawogo ama Mathew Kiongoz, Karima Chichi Mhandeni,
Engi Muro Mwanamachame, Dito Mwopao na wengineo.
Sawa kaka; umetisha
ReplyDelete