Pages

Pages

Tuesday, April 23, 2013

SHIWATA yajivunia mikakati ya kukuza na kuendeleza sanaa Tanzania

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

WASANII chipukizi 300 kutoka vikundi 15 jijini Dar es Salaam wamejitokeza kushiriki maonesho ya kukuza vipaji yaliyoandaliwa na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Jumamosi ya Aprili 27 katika ukumbi wa hoteli ya StarLight, Mnazi Mmoja Dar es Salaam, ikiwa ni mipango ya kukuza na kuendeleza sanaa.
 
Msemaji wa SHIWATA, Peter Mwenda
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa SHIWATA, Peter Mwenda, alisema kuwa vikundi ambavyo vimethibitisha kushiriki pamoja na Kaole Sanaa Group, Splendid, Uyoga Boga na vingine katika fani ya Bongo Flava, Taarab, Maigizo, Ngoma, Mazingaombwe, Sanaa za Ufundi, Kung Fu, Sarakasi, Kusheki, Kwaya na Ngonjera.

Maonesho kama haya yatafanyika kila mwezi na kiingilio ni bure na vikundi vingine ni Super Shine Morden Taarab,Zijiu,Edeneza Brass Band,Asili Africa,Mege Arts,Kintu,Army Kwanza,Wachapakazi,Tanhope,Tanz Arts,Mshikamano,Big House,Lutenga Boys,Kilimasta,Manuary.

Madhumuni makubwa ya tamasha hilo ni kuibua vipaji vya wasanii chipukizi ili kazi zao ziweze kupata soko hivyo mapromota, Majd,Maproducer wa filamu wasikoke kufika katika maonesho hayo ili kuona mastaa chipukizi ambao ambavyo vipaji vyao bado havijaonekana.

“Vijana wa sanaa mbalimbali wanatakiwa kufika katika ofisi za SHIWATA zilizopo Bungoni Ilala ili kujisajili kwa ajili ya maonesho mengine yanayofuata.

“Tanzania kuna wasanii wengi wenye vipaji lakini kazi zao hazisikiki wala kuonekana kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo ni fursa kutumia maonesho hayo kama soko la kazi zao katika jiji la Dar es Salaam,” alisema.

Wasanii mbalimbali ambao vipaji vyao vitakubalika sokoni watanufaika kupata ajira ya kuuza kazi zao pamoja na kushiriki katika matamasha mbalimbali ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment