Pages

Pages

Tuesday, April 23, 2013

Wazee wa Ngwasuma kukamua Moshi na Arusha wiki hii


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma inataraiia kufanya shoo ya aina yake mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro Alhamisi ya Aprili 25, katika Ukumbi wa Aventure, wakati Ijumaa ya Aprili 27 watakuwapo katika jijini Arusha, katika Ukumbi wa Trip A.
Baadhi ya wakali wa FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma
Shoo hizo za mwisho wa wiki hii ni sehemu ya kuwapatia burudani wapenzi wao wa Arusha na Moshi, huku wakiwa na lengo la kuonyesha makali yao katika tasnia ya muziki wa dansi nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Kelvin Mkinga, alisema kuwa wanamini shoo hizo zitawapatia burudani za aina yake mashabiki wao.

Alisema wanamuziki wao wapo kwenye kiwango cha juu kwa ajili ya kutoa burudani kamili, huku wakiamini kuwa nyimbo zao zao zitakuwa sehemu moja ya kuwapatia ladha halisi ya Ngwasuma.

“Bendi ipo imara na mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa inaendelea kuwa juu katika tasnia ya muziki wa dansi nchini kwa kuwatumia vyema waimbaji wenye vipaji vya aina yake.

“Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi katika shoo zetu hizo, ambapo ni siku mbili zenye joto la msisimko kwa wadau na wapenzi wa muziki wa dansi wa FM Academia,” alisema.

FM Academia ipo chini ya Nyosh El Saadat, akishirikiana na waimbaji mahiri akiwapo Patchou Mwamba, Pablo Masai na wakali wengine wanaotingisha katika tasnia ya muziki huo nchini.

No comments:

Post a Comment