Pages

Pages

Tuesday, April 23, 2013

Safari Lager yadhamini tena mashindano ya Pool Table, bingwa kuzoa Milioni 2.5

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa  Pool Table Tanzania (TAPA) Isaac Togocho (wa kwanza kushoto) kikombe ambacho kitashindaniwa mwaka huu, katikati ni Katibu wa chama cha Mchezo wa Pool Amos Kafwinga.
Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (katikati akiongea na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa  Pool Table Tanzania (TAPA) Isaac Togocho(wa kawanza kulia) na wa tatu kushoto niKatibu wa chama cha Mchezo wa Pool Amos Kafwinga
Nahodha wa timu ya timu ya pool inayomaliza muda wake aliyevaa shati jeupe
Oscar Shelukindo akicheza pool table
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupiti bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi kudhamini mashindano ya mchezo wa Pool Table kwa vyuo vya elimu ya juu ambayo yataanza Mei 4, mwaka huu.

Mashindano hayo yanajulikana kama “Safari Lager Higher Learning Pool Championships” yanafanyika kwa mwaka wa nne sasa na Safari Lager imekuwa wadhamini wakuu kwa miaka yote na bingwa katika mkoa atapata 500,000, wa pili 300,000 na 200,000 na mshindi kwa ngazi ya taifa atapata kikombe pamoja na 2,500,000.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana meneja wa bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo alisema nia ya kudhamini mashindano haya ni kuhamasisha wanavyuo kucheza mchezo wa pool table ikiwa ni burudani baada ya shughuli za masomo yao.

Pia alisema michezo ni muhimu kwani hupumzisha akili na kufanya warudi darasani wakiwa na ari mpya na pia hukutanisha na watu mbalimbali.
“Michezo mingi hasa pool ni burudani na husaidia akili kupumzika baada ya masomo na kufanya akili kufikiri upya na kwa ubunifu na husaidia kuwakutanisha na watu mbalimbali pia husaidia vijana watumie muda wao vizuri badala ya kujiunga na magenge yanayoweza kupotosha maadili”, alisema Shelukindo.

Naye Katibu wa chama cha Pool Tanzania (TAPA) Amos Kafwinga alisema kuwa mashindano haya yataanzia kwa vyuo kushindana katika ngazi ya mkoa na baadae mikoa yote itashindana katika ngazi ya mikoa na baadae katika ngazi ya Taifa ili kupata mshindi wa jumla kwa vyuo vyote.

Pia alisema mashindano ya mwaka huu yatahusisha vyuo vikuu vilivyo katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam na jumla ya vyuo 54 vinategemewa kushiriki

Bingwa mtetezi ni Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) cha jijini Mwanza ambao waalichukua ubingwa kwenye fainali zilizofanyika Iringa mwaka jana na fainali za mwaka huu zitafanyikajijini Dar es Salaam mwanzoni mwa Juni mwaka huu.

No comments:

Post a Comment