Pages

Pages

Tuesday, April 23, 2013

Familia yaendelea kushinikiza Wastara aendelee kupumzika nchini Omani



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MJANE wa msanii maarufu wa filamu nchini, Juma Kilowoko (Wastara Juma), ametangaza kuendelea kuishi nchini Omani kwa miezi miwili ijayo kama sehemu yake ya kujipumzisha tangu alipompoteza mume wake aliyempenda kwa dhati.
                                   Wastara kwa sasa yupo nchini Omani kwenye mapumziko
                                              Sajuki enzi za uhai wake
Wastara siku ya msiba wa mume wake
Wastara kwa sasa yupo eda ya mume wake Sajuki, aliyekufa katika Hospitali ya Muhimbili mapema mwaka huu na kushtua wadau wengi wa filamu Tanzania, kutokana na madhira yake ya ugonjwa.

Akizungumza na Handeni Kwetu, mmoja wa ndugu wa Wastara ambaye hakutaka kuliweka hadharani jina lake alisema kuwa dada yao huyo ataendelea kupumzika Omani kufikiria maisha yake zaidi.

Alisema anaamini kwa kupumzika kwa miezi miwili ijayo, itakuwa njia nzuri kwake, ukizingatia kwamba yupo kwenye kipindi kigumu tangu walipoingia kwenye mateso ya ugonjwa hadi kufariki kwa mume wake.

“Ni hali mbaya kuielezea juu ya dada Wastara, lakini kwa sasa tumeona bora kwanza hata Eda animalize akiwa huko Omani, maana Tanzania angekutana na vitu vingi vya kumuongezea machungu,” alisema.

Licha ya kutangulia mbele ya haki, Sajuki na Wastara ni miongoni mwa watu ambao wanatajwa kama wenye mapenzi ya dhati ambao Mungu pekee alifanikiwa kuwatenganisha na sio matatizo ya kidunia.

No comments:

Post a Comment