Pages

Pages

Sunday, April 14, 2013

Queen Suzy: Nyosh jamani ni baba yangu



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MALKIA wa FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, Queen Suzy, amesema kuwa anamchukulia Nyosh El Saadat kama baba yake, hivyo hawezi kujiingiza naye kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Queen Suzy akiwa na Nyosh El Saadat
Kauli ya Suzy imekuja siku chache baada ya kupigwa picha wakiwa chobingo wakibadilishana mawazo, jambo lililoibua hofu kwa wadau wa muziki wa dansi nchini.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Suzy alisema Nyosh ni baba yake hivyo wadau wasiwe na hofu naye katika suala zima la maisha yao, huku akisema kuwa faragha yao ilikuwa ni kawaida tu.

“Nyosh rais wa vijana ni baba yangu na wakati wowote naweza kukaa naye kujadili mambo ya kimaisha, hasa kwa kupitia muziki wa dansi ambao wote tupo FM Academia.

“Naamini katika hilo hakuna haja ya kujenga wasiwasi, hasa kwa kupigwa picha tunazungumza mambo yetu,” alisema Suzy.

Suzy ni miongoni mwa wasichana wanaowika katika tasnia ya muziki wa dansi nchini kwa kupitia safu ya ucheza shoo akitamba vilivyo ndani ya bendi ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma.

No comments:

Post a Comment