Pages

Pages

Sunday, April 14, 2013

Wilaya ya Kilindi kupokea tani 810 za chakula kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kupambana na njaa



Na Mwandishi Wetu, Kilindi
WILAYA ya Kilindi mkoani Tanga, inatarajia kupokea msaada wa chakula kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu jumla ya Tani 810, huku tani 80 zikipangwa kutolewa bure kwa wananchi wasiojiweza, huku kingine kikisambazwa kwa shule za Msingi na Sekondari na kinachobaki kuuzwa kwa Sh 50 kwa kilo kwa familia zenye uwezo.
Mkuu wa Wilaya Kilindi, Selemani Liwowa
Akizungumza jana mjini hapa, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa, alisema chakula hicho kinatarajiwa kuanza kuingia kesho Aprili 14 kwa ajili ya kusambazwa kwa wananchi.

Alisema kufika kwa chakula hicho ni sehemu ya serikali kupambana na njaa katika baadhi ya wilaya zilizoathiriwa na njaa, ikiwamo Kilindi, ambapo viongozi wamekuwa wakifanya juhudi kupambana nayo.

“Tunashukuru serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kutuletea chakula tanai 810 huku tukiona kuwa tutafanikiwa kwa dhati kukabiriana na suala la njaa linaloziathiri kaya mbalimbali.

“Kwa wale ambao hawana uwezo kabisa, tumewatengea tani 80, huku pia shule za msingi na sekondari zikipangwa kuwa miongoni mwa watakaokuwa kwenye msaada huu,” alisema Liwowa.

Kilindi ni miongoni mwa wilaya za Tanzania zilizokumbwa na suala la njaa, jambo linaloifanya serikali kupambana nayo kwa kupeleka msaada wa chakula wilayani hapa.

No comments:

Post a Comment