Pages

Pages

Tuesday, April 16, 2013

Queen Suzy akataa kuzaa na G-Seven kwa madai eti ni Freemason


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MNENGUAJI wa bendi ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, Queen Suzy amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kukataa kuzaa na mchumba wake anayeishi nchini Ufaransa, Aimerchard Mwamba maarufu kama G-Seven, repa wa zamani wa bendi hiyo ya FM Academia, Handeni Kwetu Blog limebaini.
G-Seven na Queen Suzy enzi za uchumba wao
Habari hizo zilijulikana juzi kuwa G-Seven alimwambia Queen Suzy ashike mimba lakini mwanadada huyo alishikwa sikio kuwa repa huyo ambaye mambo yake kwa sasa ni mazuri asithubutu kuzaa na mpenzi wake huyo kwakuwa ni Freemason.


 
Kwa raha zetu. Ndivyo walivyokuwa enzi hizo. Kwa sasa wawili hawa wapo mbalimbali, G-Seven yupo nchini Ufaransa
Habari hizo zilijulikana juzi kuwa G-Seven alimwambia Queen Suzy ashike mimba lakini mwanadada huyo alishikwa sikio kuwa repa huyo ambaye mambo yake kwa sasa ni mazuri asithubutu kuzaa na mpenzi wake huyo kwakuwa ni Freemason.

“Queen Suzy anapendwa mno na G-Seven lakini anaogopa kuzaa naye eti kwakuwa anadaiwa ni Freemason kutokana na mambo yake kuwa mazuri tangu alipohamia Ulaya.

“G-Seven mwenyewe anasema anataka kuzaa na Queen Suzy lakini yeye mwenyewe anashikwa masikio na watu ambao huenda hawana malengo mazuri na yeye,” alisema mpashaji huyo.

G-Seven  ni miongoni mwa marepa mahiri wa bendi ya FM Academia ambaye tangu aondoke pengo lake ni kubwa na amekuwa akitajwa mno na mashabiki wake.

No comments:

Post a Comment