Pages

Pages

Tuesday, April 16, 2013

Twanga Pepeta kukamua Wood Land AprilI 19 na Mei 10 Mjini Dodoma


Mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Badi Bakule Jogoo la Shamba

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
BENDI ya Twanga Pepeta ya Jijini Dar es Salaam,inatarajia kutumbuiza katika ukumbi wa Wood Land Yombo Vituka .

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya J&KK Entertainment Jane Mkumbwa alisema shoo hiyo itakua kamambe huku akiwataka wapenzi wa mziki huo kujitokeza kwa wingi ili kujionea shoo hiyo.
Jane alisema kuwa shoo hiyo itapigwa siku ya April 19 na siku kuu ya Muungano Aprili 26 itakua katika viwanja vya Kibaha Picha ya Ndege katika ukumbi wa Tripple J na huku akiwataka wananchi wa kibaha kujitokeza kwa wingi sambamba na kusherekea sikukuu hiyo.

Aliendelea kueleza kua siku ya Mei 10 mwaka huu atakuwa na bendi hiyo katika viwanja vya Bunge yaani katika jiji la Dodoma,ukumbi wa Loyal Village ambapo wabunge pamoja na wapenzi wengine wakiwemo wanavyuo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi.

"Nimeamua mei 10 kuwapelekea  wabunge burudani hivyo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi sambamba na wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kua itakua ni siku ya mapunziko ndio itakuwa sehemu sahihi ya kupumzisha vichwa vyao huo,"alisema Jane.
 
 Hata hivyo alisema kwa kushirikiana na bendi hiyo ataendelea kuwapa raha watanzania katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam, na hata mikoani.

No comments:

Post a Comment