Pages

Pages

Tuesday, April 16, 2013

DC Muhingo aendelea kumlilia Husssein Semdoe


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya Handeni, mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu, pichani chini mwenye miwani, ameendelea kumlilia marehemu Hussein Semdoe na kusema kuwa anajaribu kuwashawishi viongozi wenzake juu ya kuwakumbuka marehemu kwa kupanda miti.

Marehemu Hussein Semdoe, enzi za uhai wake
Semdoe aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi wilayani Handeni, alifariki pamoja Hassan Bwanga mwandishi wa gazeti la Uhuru na Mzalendo na Afisa Uhamiaji wilaya, Mariam Hassan.

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog kwa njia ya simu, Rweyemamu alisema kuwa vifo vyao ni pengo hivyo itakuwa jambo la busara kama wataweka utaratibu wa kuwaenzi kwa kupanda miti.

Alisema kuwa endapo jambo hilo litafanikiwa, basi utaratibu wa kupanda miti sambamba na kutunza mazingira litakuwa na faida kwa wilaya yao ambayo ina changamoto za uharibifu wa mazingira.

“Tutaendelea kumlilia Semdoe na wenzake kwa vifo vyao, ila kubwa zaidi tuwaenzi kwa vitendo kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na siku ya upandaji miti siku ya vifo vyao.

“Hili bado halikujadiliwa, ila nafikiria kuwashauri hata watu wa Misitu juu ya suala hili,” alisema Rweyemamu.

Kifo cha Semdoe na wenzake vilipokelewa kwa majonzi makubwa, vilivyotokea katika Kata ya Misima, wilayani Handeni mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment