Pages

Pages

Thursday, April 04, 2013

Naibu Waziri Angellah Kairuki atoa neno Habari Group

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki akifafanua jambo mbele ya waanzilishi wa kikundi cha Habari Group kinachojihusisha na mambo ya ujasiriamali.
 Tumeelewana jamani?
 Natoa hoja, ila siombi kura jamani... Rabia Bakari akifafanua jambo walipokutana na Angellah Kairuki.
 Rabia Bakari, mratibu wa Habari Group akimwaga maneno

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki amewataka
wanachama wa kikundi cha waandishi wa habari cha kujikomboa
kiuchumi (Habari Group) kupendana na kuaminiana ili kukifikisha
kikundi hicho mbali.

Kairuki ambaye pia ni mlezi wa Habari Group, alikitaka kikundi hicho
kutokuwa wachoyo wa kusaidia waandishi wa habari wengine wenye nia ya kuungana na kufanikiwa kimaisha.


 Tabasamu lilitawala namna hii


Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki, akizungumza na waanzilishi wa kikundi cha Habari Group kinachojihusisha na mambo ya ujasiriamali. Kulia kwake ni dada mlezi wa kikundi hicho, Joketi Mwigelo.

Akizungumza na kikundi hicho Dar es Salaam juzi, alisema ili mtu
afanikiwe ni lazima awe mwenye upendo na kusaidia wengine pale
penye mwanya wa kufanya hivyo na kuwataka wanachama wote kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya kikundi.

"Sitopenda kusikia kikundi hiki kimekufa kwa sababu ya mifarakano na chuki miongoni mwenu kwani kwa kufanya hivyo hamtofikia malengo
mliyokusudia," alisema Kairuki.

 Aliongeza kuwa wakati anaingia madarakani aliweka vipaumbele kwa
 wafanyakazi wa majumbani, madereva wa aina zote, wafanyakazi wa
 mashambani, wahudumu wa baa na nyumba za wageni, walinzi na
 waandishi wa habari.

 Na kwamba ameanza kushughulikia haki mbalimbali za makundi hayo,
 ambapo kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuishinikiza serikali
 kusaini mkataba wa kuridhia haki za wasichana wa majumbani.

Aliwapongeza waandishi wa habari kwamba pamoja na changamoto
nyingi wanazokutana nazo, lakini hawakati tamaa na wamekuwa
wakifanya kazi yao kwa moyo mmoja na kwa bidii.

Kama mkakati wake wa kuwasaidia waandishi wa habari, alisema
atasimamia Habari Group ili wawe mabalozi wazuri kwenye mambo
mbalimbali kwa jamii, ikiwemo kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali,
kuwapa elimu ya umuhimu wa cheti cha kuzaliwa, sambamba na
kushirikiana nao bega kwa bega kwenye mambo muhimu ya kijamii.

"Kuwasidia kwenu ni miongoni mwa malengo yangu niliyojiwekea ya
kupigania haki ya baadhi ya makundi ambyo nimeona haki zao kama
wafanyakazi hazitekelezwi,"aliongeza.



No comments:

Post a Comment