Pages

Pages

Tuesday, April 23, 2013

Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam yaendelea kushika kasi


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
LIGI Darajala la Pili Mkoa wa Dar es Salaam , hatua ya sita bora imezidi kushika kasi ambapo hadi sasa timu ya Red Coast inaongoza ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 7 baada ya kucheza mechi tatu.
Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Mharizo, Red Coast imejikusanyia pointi hizo baada ya kuzifunga  Abajalo bao 1-0,  huku ikilazimishwa sare ya bila kufungana na Friends Rangers na jana Jumatatu iliichapa Sharif mabao 3-1, katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Airwing.

Friends Rangers wanashika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 5, ilizozivuna kwa kutoka sare ya bila kufungana na Day Break katika mechi ya kwanza, kasha kulazimishwa  tena sare ya bila kufungana na  Red Coast na jana Jumatau iliifunga Boom FC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa.

Abajao inashiaka nafasi ya tatu ikiwa na pointi 4, huku Sharif Star ikishika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 3, ikifuatiwa na Day Break yenye pointi 3 wakati Boom FC ikiburuza mkia kwa kuwa na pointi 1.

Kesho Jumatano ligi itaendelea kwa michezo mitatu, Abajalo vs Friends Rangers uwanja wa Kinesi, Red Coast vs Boom uwanja wa Makurumla na Sharif Stars vs Day Break uwanja wa Airwing, huku Ligi hiyo  ikitarajiwa kumalizika Aprili 27 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment