Pages

Pages

Monday, March 25, 2013

Wema amfanyia kufuru Kajala kwa kumlipia Milioni 13

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSANII Wema Sepetu amefanya kufuru kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 msanii mwenzake, Kajala Masanja na kumfanya awe huru katika kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na mumewe
Kajala Masanja.
Mapema leo, Kajala alihukumiwa kwenda jela miaka 5 au kulipa faini ya shilingi milioni 13, huku ikiwa ni kesi ambayo tayari ilishakuwa ngumu kwa mwanadada huyo.

Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na tuhuma za kutakatisha fedha haramu.

Faraji yeye amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 213, huku mke wake akinusurika zaidi baada ya kutofaini yake na Wema Sepetu.

Kwa sasa Kajala yupo nyumbani kwao maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam pamoja na ndugu na jamaa.

No comments:

Post a Comment