Pages

Pages

Tuesday, March 26, 2013

Tenga ataka umri sahihi michuano ya Copa Coca-Cola 2013

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewataka viongozi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhakikisha wanaingiza wachezaji wenye umri sahihi katika michuano ya U15 FIFA Copa Coca-Cola 2013.
Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Ametoa mwito huo leo (Machi 26 mwaka huu) wakati akifungua semina elekezi ya michuano ya Copa Coca-Cola ambayo kuanzia mwaka huu itakuwa ikishirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15.


Rais Tenga amesema hakuna jambo la kipuuzi kama kuchomekea wachezaji ambao wamezidi umri unaotakiwa kwa vile lengo la michuano ya aina hiyo ni kubaini vipaji na kuwafanya watoto wapende kucheza mpira wa miguu.

“Kwanza nawashukuru kwa kutenga muda wenu na kuhudhuria semina. Lakini ni vizuri pia mkahakikisha mnakuwepo kwenye mashindano ili kutekeleza haya ambayo tutakubaliana katika semina hii. Mkileta mtu mwingine anaweza kutuanzishia mambo mengine badala ya yale tutakayokubaliana,” amesema Tenga.

Pia ameishukuru kampuni ya Coca-Cola ambaye imekuwa ikidhamini michuano hiyo tangu mwaka 2007 ambapo semina hiyo elekezi inayoshirikisha makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na waratibu wa mikoa wa michezo ya UMISSETA ni ya saba mfululizo.

Ratiba ya michuano hiyo kuanzia mwaka huu imebadilika ambapo sasa itaanzia ngazi ya wilaya Aprili wakati fainali katika ngazi ya Taifa itachezwa Septemba.



No comments:

Post a Comment