Pages

Pages

Monday, March 25, 2013

Green Stone watakiwa waisaidie Yanga



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MLEZI wa tawi la Yanga la Green Stone, Yusuph Shaban Mhandeni maarufu kama (Yusuphed Mhandeni), amewataka wanachama wa tawi lao kujenga dhamira ya kweli ya kuisaidia klabu yao pamoja na kujikomboa wenyewe kwa kuhakikisha kuwa muungano unakuwa na tija.
Yusuphed Mhandeni

Green Stone ni tawi lililoanzishwa mwishoni mwa mwaka jana, huku tayari likianza kutambulika kutokana na uongozi wa Yanga, kuanza kugawa kadi mpya kwa wanachama walioomba kupitia tawi hilo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mhandeni alisema kuwa endapo tawi hilo litakuwa na mapenzi ya kweli kwa klabu yao, pamoja na wao kuungana kwa kujikomboa kiuchumi, mambo yao yatakuwa mazuri.

Alisema tawi lenye muunganiko wa kweli, litawafanya wanachama kuweza kujadili mambo yenye tija, yakiwamo mguso wa utafutaji na kusaidiana kwa namna moja ama nyingine na sio kuwaza mambo yasiyokuwa na maana.

“Tunashukuru kwa kuanzisha tawi hili lenye ari kubwa ya kuhakikisha kwamba baada ya siku chache zijazo, Green Stone linakuwa kwenye macho na masikio ya kila wadau wa michezo.

“Naamini hali hiyo itawasaidia wanachama wote, ndio maana nimeamua kuwa karibu nao kwa kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda sawa, hasa kwa kusaidiana na sio kuwaza yale yasiyokuwa na tija na kuiathiri klabu yetu,” alisema.

Wiki iliyopita, tawi hilo liligawa kadi tano kwa wanachama wao waliopewa na klabu yao, huku wakiomba kwa kupitia Green Stone, kuashiria kuwa sasa limeanza kutambulika kama yanavyotambuliwa matawi mengine.

No comments:

Post a Comment