Pages

Pages

Wednesday, March 06, 2013

Wazee wa Ngwasuma waipania shoo ya Mango Garden Ijumaa


Wanenguaji wa FM Academia, Wazee wa Ngwasuma

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, wanatarajia kufanya onyesho la nguvu katika Ukumbi wa Mango Garden, Ijumaa kwa ajili ya kuwapatia burudani za aina yake mashabiki wao katika tasnia hiyo ya muziki wa dansi.

Rais wa Vijana, Nyosh El Sadaat

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais wa bendi hiyo, Nyosh El Sadaat, alisema kwamba shoo hiyo itakuwa ya aina yake kutokana na umahiri wao katika tasnia ya muziki wa dansi nchini.

Alisema vijana wake wote wapo tayari kwa mashambulizi yao katika viwanja hivyo vya Mango Garden, hivyo anaamini wadau na mashabiki watakaokuja kwenye shoo hiyo watapata kile kinachostahili kutoka kwao.

“FM Academia sio bendi ya mzaha mzaha, hivyo wadau wetu waje kwa wingi katika Ukumbi huo kujionea namna gani sisi tupo juu na hatuna mpinzani kwa sasa, huku tukiwa na nyimbo nyingi zinazopendwa na watu wengi.

“Naamini tutakuwa imara zaidi, huku nikiwapanga wanamuziki wenzangu kwa ajili ya kuonyesha umahiri wetu katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini,” alisema.

Wazee wa Ngwasuma wanatamba na nyimbo zao nyingi, ukiwamo ule wa Heshima kwa Mwanamke, Otilia na nyinginezo zinazofanya vyema katika kumbi mbalimbali za burudani, ukiwamo ule wa Kijiji cha Makumbusho kila Jumamosi na New Msasani Club, kila Jumapili.

No comments:

Post a Comment