Pages

Pages

Wednesday, March 06, 2013

Uchaguzi Mkuu Kenya: Utaratibu wa kuhesabu kura kwa mkono waanza, Odinga aongoza kura za Afrika Mashariki



Uhuru Kenyatta

Na Mwandishi Wetu, Kenya
UCHAGUZI Mkuu Kenya, uliofanyika juzi, umeingia katika sura mpya, baada ya mtambo wa kuhesabia kura kuendelea kusumbua, hivyo kulazimika Tume Huru ya Uchaguzi huo nchini hapa kuagiza utaratibu wa kuhesabu kwa mkono kuanza.
Raila Odinga

Hata hivyo, matokeo yanaendelea kuwa juu kwa mgombea Uhuru Kenyatta, akiafutiwa na Raila Odinga, mgombea ambaye kwa Tanzania, watu wengi wameonekana kumuunga mkono.

Tume Huru ya Uchaguzi nchini hapa, iliagiza kura zihesabiwe kwa mkono katika vituo vya uchaguzi na kuletwa hapa Bomas of Kenya, sehemu ambayo imeweka Makao Makuu ya muda.

Mtambo huo ulianza kukorofisha tangu jana ambapo ilisababisha kuhesabu moja kwa moja kushindikana, jambo ambalo huenda likawa changamoto kubwa katika uchaguzi huu.

Tangu watangaze rasmi kwamba kura zitahesabiwa kwa mkono mida ya saa saba ni majimbo matatu tu ambayo matokeo yake yametoka mpaka sasa.

Katika hali ya kuongeza msisimko katika Uchaguzi huo hapa nchini, Wakenya waliopiga kura katika nchi za Afrika Mashariki wamemchagua Odinga kwa Kura 1224, wakati Kenyata amepata kura 951.

No comments:

Post a Comment