Pages

Pages

Thursday, March 07, 2013

Upepo waendelea kuvuma upande wa Uhuru Kenyatta, Uchaguzi Kenya



Uhuru Kenyatta

Na Mwandishi Wetu, Kenya
WAKATI Mgombea Urais wa ODM, Raila Odinga, akitarajiwa kukutana na wanahabari leo, matokeo ya Uchaguzi huo ni Uhuru Kenyatta anaongoza kwa kura 2,416,321, akifuatiwa na Odinga mwenye kura 1,880,908. 102.

Matokeo ya kura hizo ni zimekuja baada ya kuaanza kuhesabiwa kwa kutumia mkono, baada ya mtambo uliokuwa ukitumika tangu Jumatatu kusitishwa baada ya kubainika kuwa umeharibika.

Hata hivyo, bado Uchaguzi huo umekuwa na mvuto pamoja na ushindani wa aina yake kwa wagombea wawili, Kenyatta na Odinga, ambaye ni Waziri Mkuu katika serikali ya Mwai Kibaki, inayolekea mwishoni mwaka huu.

Matokeo zaidi ya uchaguzi huo yataendelea kutolewa kadri yatakavyoendelea kupatikana.

No comments:

Post a Comment